Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Saturday, September 4, 2010

ALGERIA NA TANZANIA ZATOKA SARE YA 1-1

Timu ya Taifa ya Tanzania imetoka sare na timu ya taifa ya Algeria, Tanzania ndiyo ilikuwa ya kwanza kupachika bao kwa njia ya mpira wa adhabu.Algeria walisawazisha baadaye kwa shuti la mbali ambalo lilimshinda kipa wa Tanzania.

Goli la Tanzania lilifungwa na Abdi Kassim.

Saturday, May 8, 2010

Toronto Fc yazima Chicago Fire

Toronto Fc imeichapa timu ya Chicago Fire kwa mabao 4-1, mchezo huo ulikuwa leo katika kiwanja cha BMO field jijini Toronto.Kwa ushindi huu Toronto bado inashikilia rekodi yake ya kutofungwa kwenye uwanja wa nyumbani tokea msimu huu uanze. Chad Barrett aliongoza katika magoli baada ya kupachika magoli 2 dhidi ya timu yake ya zamani, magoli mengine yalipachikwa na O'brien white pamoja na Nick labrocca. Toronto watacheza na Monteal Impact tarehe 12 May. Picha na TFC website.

Man U na Celtic kucheza Toronto July 16

MIGHTY Man U aka THE RELIGION CELTIC FC Timu za Manchester United ya Uingereza na Celtic ya Scotland, zinatarajia kupambana Jijini Toronto katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika tarehe 16 Julai mwaka huu. Mpambano huo wa kirafiki utafanyika katika uwanja wa Rogers centre zamani ikiitwa Sky Dome, pambano hilo linatarajiwa kuanza saa mbili za jioni siku hiyo ya ijumaa. Tiketi zitapatikana kupitia mtandao au wakala wa Ticketmaster popote walipo. Viingilio katika mpambano huo vitakuwa ni dola 75 mpaka 150 na tiketi zitauzwa siku ya tarehe ishirini mwezi Mei, kwa wale wapenzi wa mpira kazi kwenu. Esmail.

Sunday, April 25, 2010

Simba Sc Wawafunga El Hadoud

Timu ya simba pichani iliyowafunga wamisri Haras Al Hadoud mabao 2-1 katika Uwanja wa taifa leo hii.Mabao ya Simba yalifungwa na Mgosi na Okwi.