Timu ya simba pichani iliyowafunga wamisri Haras Al Hadoud mabao 2-1 katika Uwanja wa taifa leo hii.Mabao ya Simba yalifungwa na Mgosi na Okwi.
Sunday, April 25, 2010
Simba Sc Wawafunga El Hadoud
Timu ya simba pichani iliyowafunga wamisri Haras Al Hadoud mabao 2-1 katika Uwanja wa taifa leo hii.Mabao ya Simba yalifungwa na Mgosi na Okwi.
Saturday, April 24, 2010
Thursday, April 22, 2010
BINTI WA KITANZANIA APOTEA
| Toronto Police Service News Release |
Wednesday, April 21, 2010 - 12:18 PM
33 Division
416-808-3300 The Toronto Police Service is requesting the public's assistance locating a missing woman. Elizabeth Chirwa, 22, was last seen on Tuesday, April 20, 2010, at 6:30 a.m., in the area of Graydon Hall Drive. She is described as black, 5'3", 141 lbs, with straight, black hair in a ponytail. She may be carrying a small, black handbag. Police are concerned for her safety. Anyone with information is asked to contact police at 416-808-3300, Crime Stoppers anonymously at 416-222-TIPS (8477), online at www.222tips.com, or text TOR and your message to CRIMES (274637). Constable Isabelle Cotton, Public Information, for Detective Brian Martell, 33 Division
Washiriki wa Miss Universe Tanzania 2010
Tabia toka Dodoma
Selina toka Dar
Sanje toka Dodoma
Redempta toka Moro
Rose toka Dodoma
Neema
Nasra toka Dar
Mwajabu toka Mwanza
Maureen toka Moro
Mary toka Moro
Josephine toka Dar
Immaculata toka Mwanza
Halima toka Arusha
Fatma toka Dar
Gaudencia toka Moro
Esther toka Mwanza
Devota toka Dar
Demitria toka Dar
Anna toka Dar
Hellen toka Arusha- ameibuka mshindi wa Miss universe Tanzania
Wednesday, April 21, 2010
Mbunge wa Wawi Pemba na Kiongozi wa upinzani katika bunge la Tanzania Mh. Hamad Rashid, alikutana na watanzania waishio katika jiji la Toronto na vitongoji vyake.Mkutano huo ulifanyika jumamosi ya terehe 17 ambapo mheshimiwa Hamad alipata fursa ya kusalimiana na kubadilishana mawazo ikiwa pamoja na kujibu maswali.
Kama ilivyo kwa viongozi wengine waliomtangulia Mheshimiwa alisisitiza umuhimu wa wazawa wa Tanzania kurudi nyumbani kuwekeza, alisema kuwa anafahamu kwamba bado kuna vikwazo lakini tusikate tamaa. Akitoa mfano alisema, yeye ameshafungua biashara ya uvuvi, usafiri wa anga bila mafanikio makubwa lakini bado hajakata tamaa.
Akijibu maswali Mheshimiwa alisema suala la uraia wa nchi mbili lipo katika hatua za mwisho kwani hata mipaka ya jumuia ya Afrika mashariki itafunguliwa mwakani (2011), vilevile akijibu tuhuma kuwa yeye amenunuliwa na chama tawala (CCM) alisema tuhuma hizo si za kweli na yeye alikuwa mtu wa kwanza kuzungumzia na kukemea tuhuma zilizohusisha mikataba mibovu.
Mwisho alisisitia kuwa yeye ni mtu safi ila huwa hapendi kukabiliana na matatizo kwa njia ya ugomvi, kashfa au matusi.Alimalizia kwa kusema baba yake aliwahi kumwambia kuwa kama mtu akimtuhumu kwa uchawi wakati si kweli basi hana sababu ya kuogopa.
Mheshimiwa Hamad Rashid alisafiri baadeye jioni kuendelea na ziara yake kuelekea BC.
TANESCO KUONGEZA MTANDAO WA UMEME MBINGA
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima akiongea na waandishi wa habari.
Benjamin Sawe: Maelezo Dodoma
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la umeme nchini imepanga kuongeza mtandao wa umeme mjini Mbinga kwa kujenga ujenzi wa njia ya kilometa moja ya msongo wa KV 11.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima alisema ingawa Mbinga imeshapata umeme wa jenereta mbili zenye uwezo wa kuzalisha jumla ya MW2.5 bado kunahitajika umeme zaidi kulingana na shughuli za kiuchumi na jamii kuwa juu
Alisema Tanesco pia itafunga transoma yenye uwezo wa KVA 100 ikiwa ni pamoja na kujenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 2.0 ili kusambaza umeme maeneo ya Matika Tanki la maji mjini Mbinga.
Kwa mujibu wa Mheshimiwa Malima pia itafungwa transofoma yenye uwezo wa KVA 100 na kujenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 2.0 ili kusambaza umeme katika maeneo ya Matarawe Ruhuwiko
Aidha Mheshimiwa Malima alisema Serikali itajenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 1.5 ili kusambaza umeme maeneo ya kiwandani Mbambi.
Alisema tatizo linalokwamisha upelekaji wa maeneo ya Maguu,Litembo,Matiri na Ruanda ni uwezo mdogo wa Serikali wa kutekeleza miradi ya kusambaza umeme nchi yote kwa pamoja kulingana na uwezo wa fedha.
Hivyo amewahakikishia wananchi kwamba Serikali itaendelea na juhudi za kutafuta fedha za kufikisha umeme kwa viwango bora zaidi katika vijiji vya Maguu Litembo,Matiri na Ruanda kuliko ilivyo hivi sasa
Subscribe to:
Posts (Atom)
