Sunday, October 10, 2010

ARI MPYA

Wanachama wa TCA pamoja na Viongozi wanaomaliza muda wao kwa pamoja, wamemchagua ndugu Patrick Kamera kuwa msimamizi wa uchaguzi mkuu ujao.

Ndugu Kamera ni mwanachama wa siku nyingi TCA na kazi yake kubwa itakuwa ni kuandaa tarehe ya uchaguzi, mahala pa kufanyia uchaguzi ikiwa pamoja na jinsi ya kufanya uchaguzi.

Katika mkutano huo mambo mengi yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba ambayo inatakiwa iendane na mahitaji ya wanachama katika muda huu,vilevile wanachama walipendekeza mawazo mbali mbali ambayo yatapelekea chama kuwa na muelekeo mpya,ikiwa ni pamoja kuendeleza yote mazuri ambayo yamefanywa na uongozi unaomaliza muda wake.

Mkutano huo ulichukua pia nafasi ya kupendekeza majina ya baadhi ya wanachama ambao inadhani wana nia na uwezo wa kushika nafasi mbali mbali za uongozi, tarehe na taratibu zitakazofuata zitatangazwa hapo baadaye.

Kwa ufahamu tu TCA ilianzishwa mwaka 1990 na watanzania wachache ambao waliona umuhimu wa kuwa na jumuia ambayo itawaweka pamoja wahamiaji toka Jamhuri ya muungano wa Tanzania, mpaka muda huu TCA ina miaka Ishirini.

Walioketi ni viongozi wanaomaliza muda wao na nyuma yao ni viongozi wanaotarajiwa kuingia madarakani, mwenye mvi ni mmoja wa waanzilishi na mstaafu Mzee Omari Mwinyi.

No comments: