Wednesday, April 21, 2010

Mbunge wa Wawi Pemba na Kiongozi wa upinzani katika bunge la Tanzania Mh. Hamad Rashid, alikutana na watanzania waishio katika jiji la Toronto na vitongoji vyake.Mkutano huo ulifanyika jumamosi ya terehe 17 ambapo mheshimiwa Hamad alipata fursa ya kusalimiana na kubadilishana mawazo ikiwa pamoja na kujibu maswali.
Kama ilivyo kwa viongozi wengine waliomtangulia Mheshimiwa alisisitiza umuhimu wa wazawa wa Tanzania kurudi nyumbani kuwekeza, alisema kuwa anafahamu kwamba bado kuna vikwazo lakini tusikate tamaa. Akitoa mfano alisema, yeye ameshafungua biashara ya uvuvi, usafiri wa anga bila mafanikio makubwa lakini bado hajakata tamaa.
Akijibu maswali Mheshimiwa alisema suala la uraia wa nchi mbili lipo katika hatua za mwisho kwani hata mipaka ya jumuia ya Afrika mashariki itafunguliwa mwakani (2011), vilevile akijibu tuhuma kuwa yeye amenunuliwa na chama tawala (CCM) alisema tuhuma hizo si za kweli na yeye alikuwa mtu wa kwanza kuzungumzia na kukemea tuhuma zilizohusisha mikataba mibovu.
Mwisho alisisitia kuwa yeye ni mtu safi ila huwa hapendi kukabiliana na matatizo kwa njia ya ugomvi, kashfa au matusi.Alimalizia kwa kusema baba yake aliwahi kumwambia kuwa kama mtu akimtuhumu kwa uchawi wakati si kweli basi hana sababu ya kuogopa.
Mheshimiwa Hamad Rashid alisafiri baadeye jioni kuendelea na ziara yake kuelekea BC.

No comments: