Wednesday, April 21, 2010

TANESCO KUONGEZA MTANDAO WA UMEME MBINGA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima akiongea na waandishi wa habari. Benjamin Sawe: Maelezo Dodoma Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la umeme nchini imepanga kuongeza mtandao wa umeme mjini Mbinga kwa kujenga ujenzi wa njia ya kilometa moja ya msongo wa KV 11. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima alisema ingawa Mbinga imeshapata umeme wa jenereta mbili zenye uwezo wa kuzalisha jumla ya MW2.5 bado kunahitajika umeme zaidi kulingana na shughuli za kiuchumi na jamii kuwa juu Alisema Tanesco pia itafunga transoma yenye uwezo wa KVA 100 ikiwa ni pamoja na kujenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 2.0 ili kusambaza umeme maeneo ya Matika Tanki la maji mjini Mbinga. Kwa mujibu wa Mheshimiwa Malima pia itafungwa transofoma yenye uwezo wa KVA 100 na kujenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 2.0 ili kusambaza umeme katika maeneo ya Matarawe Ruhuwiko Aidha Mheshimiwa Malima alisema Serikali itajenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 1.5 ili kusambaza umeme maeneo ya kiwandani Mbambi. Alisema tatizo linalokwamisha upelekaji wa maeneo ya Maguu,Litembo,Matiri na Ruanda ni uwezo mdogo wa Serikali wa kutekeleza miradi ya kusambaza umeme nchi yote kwa pamoja kulingana na uwezo wa fedha. Hivyo amewahakikishia wananchi kwamba Serikali itaendelea na juhudi za kutafuta fedha za kufikisha umeme kwa viwango bora zaidi katika vijiji vya Maguu Litembo,Matiri na Ruanda kuliko ilivyo hivi sasa

No comments: