Tuesday, April 20, 2010

SHUKURANI

Familia ya Mzee Gembe wa Upanga Dar-es-salaam na Tabora,kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu,jamaa,majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu mtoto wetu,mdogo wetu,dada yetu, Evaline Gembe ambaye alifariki huko Toronto nchini Canada katika hospitali ya Mtakatifu Michael tarehe 30/March/2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 13/Aprili/2010 kijijini Inyonga Mkoa wa Tabora.

Shukrani za pekee tunaomba ziwafikie Jumuiya yote ya watanzania wanaoishi nchini Canada hususani katika Jiji la Toronto na vitongoji vyake. Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili hadi kuusafirisha kwa gharama kubwa kutoka Toronto hadi Dar-es-salaam mnamo tarehe 8/April/2010.Asanteni kwa sala,maombi na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu.Shukrani za pekee ziwaendee kamati nzima iliyoratibu na kufanikisha shughuli nzima ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Evaline kuja Tanzania.

Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani Dar-es-salaam na Tabora katika kutufariji,mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia zingine kwa nia ya kutufariji na kututia nguvu.Asanteni sana.

Shukrani pia ziuendee Ubalozi wa Tanzania nchini Canada na Jumuiya mbalimbali za ki-Tanzania nchini Marekani na wanablogu wote waliolitoa tangazo la kifo kwenye Blogu zao.

Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee,tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa ndugu yetu Evaline.Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.

Sisi tulimpenda sana Evaline lakini

Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,

Jina la Bwana lihimidiwe.

Amen

1 comment:

Anonymous said...

R.I.P Eve!


MG