Saturday, May 8, 2010

Man U na Celtic kucheza Toronto July 16

MIGHTY Man U aka THE RELIGION CELTIC FC Timu za Manchester United ya Uingereza na Celtic ya Scotland, zinatarajia kupambana Jijini Toronto katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika tarehe 16 Julai mwaka huu. Mpambano huo wa kirafiki utafanyika katika uwanja wa Rogers centre zamani ikiitwa Sky Dome, pambano hilo linatarajiwa kuanza saa mbili za jioni siku hiyo ya ijumaa. Tiketi zitapatikana kupitia mtandao au wakala wa Ticketmaster popote walipo. Viingilio katika mpambano huo vitakuwa ni dola 75 mpaka 150 na tiketi zitauzwa siku ya tarehe ishirini mwezi Mei, kwa wale wapenzi wa mpira kazi kwenu. Esmail.

2 comments:

Anonymous said...

Dah lazima nkawaone Man U Live, Ahsante sana kaka angu kwa info hii maana dah

tca said...

Hii kitu itakuwa safi sana!