Saturday, May 8, 2010

Toronto Fc yazima Chicago Fire

Toronto Fc imeichapa timu ya Chicago Fire kwa mabao 4-1, mchezo huo ulikuwa leo katika kiwanja cha BMO field jijini Toronto.Kwa ushindi huu Toronto bado inashikilia rekodi yake ya kutofungwa kwenye uwanja wa nyumbani tokea msimu huu uanze. Chad Barrett aliongoza katika magoli baada ya kupachika magoli 2 dhidi ya timu yake ya zamani, magoli mengine yalipachikwa na O'brien white pamoja na Nick labrocca. Toronto watacheza na Monteal Impact tarehe 12 May. Picha na TFC website.

No comments: