Monday, November 29, 2010
Sunday, November 28, 2010
REAL MADRID FC KUPAMBANA NA BARCELONA FC -KESHO
Lile pambano linalosubiriwa kwa hamu la miamba ya soka nchini Hispania,Real Madrid na Barcelona, limewadia. Zikiwa zimebakia saa chache wachezaji wa pande zote mbili wanaashiria kutoogopa timu pinzani au mpambano huo kwa ujumla.
Real Madrid chini ya kocha Jose Mourinho, inaingia kwenye pambano hilo ikiwa haijapoteza mchezo kwa kushinda mechi kumi na sare mbili.Kwa upande wa Barcelona wao wana rekodi ya kushinda mechi kumi sare moja na kupoteza mchezo mmoja.
Kukiwa hakuna majeruhi kwa pande zote mbili, mpambano huo unatarajiwa kuwa mkali kwani kumbukumbu zinaonyesha, toka walipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 1902, Madrid imeshinda mara 85 na Barcelona 81 huku kukiwa na sare 42.
Mchezaji nyota wa Real Madrid, Christiano Ronaldo amesema wao wanakwenda Camp Nou kwa nia ya kutafuta ushindi na si vinginevyo wakati Lionel Messi,mshambuliaji hatari wa Barcelona, raia wa Argentina, alikaririwa akisema hivi karibuni kwamba Barcelona bado ni timu bora kuliko wapinzani wao, ingawa anakubali kuwa bidii na moto wa Madrid mwaka huu ni tofauti na misimu miwili iliyopita.
Mourinho anatarajia kupunguza “uteja” wa Madrid kwa Barcelona chini ya Guardiola, wakati Mourinho akitamba kuujua mpambano huo hata akiwa usingizini.Madrid hawajaifunga Barcelona nyumbani toka desemba ya 2007 na Mourinho ameshaifunga Barcelona akiwa kocha wa Chelsea na Inter Milan.Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kocha Jose Mourinho kuiongoza Real Madrid katika mpambano na Barcelona.
Ushindi katika El Classico unachukuliwa kuwa ni ishara ya ushindi wa ligi kwani katika misimu sita iliyopita, mshindi wa mpambano huu ndiye aliyechukua kombe mwisho wa msimu.Jumla ya mashabiki 98,000 wanatarajiwa kushuhudia mpambano huo ndani ya Uwanja wa nyumbani wa Barcelona,Nou Camp,huku mamilioni ya mashabiki wa soka ulimwenguni wanatarajiwa kuufuatilia mpambano huo kupitia luninga na mtandaoni.

Nyota wa pande zote mbili wamekuwa na ari ya kutaka kuonyesha vipaji na uwezo wao wakati Ronaldo na Messi wakimimina mvua za magoli katika mechi za karibuni.Huu unaaminika kuwa pia mpambano baina ya Ronaldo na Messi katika kuonyesha nani ni bora zaidi miongoni mwao.
Zote hizi ni dondoo tu, mpira huchezwa kwa dakika tisini.Tusubiri matokeo.
Written by E.Manambi with additional notes by Jeff Msangi
Wednesday, November 24, 2010
Baraza la Mawaziri la Serikali ya Tanzania -2010
OFISI/WIZARA | WAZIRI | ||
1. | Ofisi ya Rais | 1. WN – OR – Utawala Bora Mathias Chikawe 2. WN – OR – Mahusiano na Uratibu Stephen Wassira | |
2. | Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma | Hawa Ghasia | |
3. | Ofisi ya Makamu wa Rais | 1. Muungano Samia Suluhu 2. Mazingira Dr. Terezya Luoga Hovisa | |
4. | Ofisi ya Waziri Mkuu | 1. Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi 2. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu | |
5. | Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | George Huruma Mkuchika Naibu-Aggrey Mwanri Naibu-Kassim Majaliwa | |
6. | Wizara ya Fedha | Mustapha Mkulo Naibu-Gregory Teu Naibu-Pereira Ame Silima | |
7. | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | Shamsi Vuai Nahodha Naibu-Balozi Khamis Suedi Kagasheki | |
8. | Wizara ya Katiba na Sheria | Celina Kombani | |
9. | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa | Bernard K. Membe Naibu-Mahadhi Juma Mahadhi | |
10. | Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa | Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi | |
11. | Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi | Dr. Mathayo David Mathayo Naibu-Benedict Ole Nangoro | |
12. | Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia | Prof. Makame Mnyaa Mbarawa Naibu-Charles Kitwanga | |
13. | Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi | Prof. Anna Tibaijuka Naibu-Goodluck Ole Madeye | |
14. | Wizara ya Maliasili na Utalii | Ezekiel Maige | |
15. | Wizara ya Nishati na Madini | William Mganga Ngeleja Naibu-Adam Kigoma Malima | |
16. | Wizara ya Ujenzi | Dr. John Pombe Magufuli Naibu-Dr.Harrison Mwakyembe | |
17. | Wizara ya Uchukuzi | Omari Nundu Naibu-Athumani Mfutakamba | |
18. | Wizara ya Viwanda na Biashara | Dr. Cyril Chami Naibu-Lazaro Nyalandu | |
19. | Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi | Dr. Shukuru Kawambwa Naibu- Philipo Mulugo | |
20. | Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii | Dr. Haji Hussein Mpanda Naibu-Dr Lucy Nkya | |
21. | Wizara ya Kazi na Ajira | Gaudensia Kabaka Naibu-Makongoro Mahanga | |
22. | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto | Sophia Simba Naibu-Umi Ali Mwalimu | |
23. | Wizara ya Habari, Vijana na Michezo | Emmanuel John Nchimbi Naibu-Dr Fenella Mukangara | |
24. | Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki | Samuel John Sitta Naibu-Dr. Abdalah Juma Abdallah | |
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika | Prof. Jumanne Maghembe Naibu-Christopher Chiza | ||
26. | Wizara ya Maji | Prof. Mark James Mwandosya Naibu-Eng. Gerson Lwinge |
Monday, November 15, 2010
Matokeo ya Uchaguzi-TCA
Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCA kwa pamoja walichagua viongozi wao wa jumuia kulingana na matakwa ya katiba. Zifuatazo ni picha na majina ya viongozi wapya.
Aliko Mwakatobe-Mwenyekiti
Patrick Kamera-Katibu
Yasmin Kassam-Mweka Hazina
Richard Mwakijale-Mwenyekiti Vijana
Rami Hamisi-Mwenyekiti Uanachama
Adam Kasela-Mwenyekiti Jamii/Starehe
Dr Donatus Mutasingwa-Mwenyekiti Elimu
Wajumbe wa mkutano mkuu na viongozi wapya.
Aliko Mwakatobe-Mwenyekiti
Patrick Kamera-Katibu
Yasmin Kassam-Mweka Hazina
Richard Mwakijale-Mwenyekiti Vijana
Rami Hamisi-Mwenyekiti Uanachama
Adam Kasela-Mwenyekiti Jamii/Starehe
Dr Donatus Mutasingwa-Mwenyekiti Elimu
Wajumbe wa mkutano mkuu na viongozi wapya.
Monday, November 1, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)